Saturday, 14 January 2017

FAHAMU MAFUNZO YA UFUGAJI WA NYUKI

Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatul,ni matumaini yangu wote tu wazima alhamdulillah 
Leo katika darasa tutajifunza kuhusuana na ufugaji wa nyuki
Naam,kwa kawaida makundi ya nyuki katika nchi ya Tanzania na baadhi ya nchi zinazolingana kwa tabia za nchi, makundi ya nyuki huanza kutafuta sehemu salama na yenye chakula kwa wingi kuanzia mwezi wa kumi katika mwaka mpaka mwezi wa nne kwa mwaka unaofuata.Kipindi hiki huwa na makundi mengi yanayozunguka hapa na pale kutafuta nyumba ambayo itawafaa kwa ajili ya makazi yao na kwa ajili ya kuhifadhia chakula.

Hiki ndio huwa kipindi muafaka sana kwa wafugaji kuanza kutega mizinga ambayo imeshaandaliwa kwa ajili ya kufugia nyuki.Kwa kuwa makundi mengi huwa yanatafuta sehemu za makazi hivyo ni rahisi sana kuyakama na kuyahifadhi makundi hayo kwa ajili ya uzalishaji wa mazao ya nyuki.

Kutokana na hilo, mfugaji anapaswa kuanza kuandaa sehemu ya kufugiua nyuki na mizinga yake mapema zaidi kabla ya msimu huo kufika ili asiweze kukosa makundi ya nyuki.Unashauriwa kuanza kuandaa mazingira ya kufugia nyuki na mizinga angalau mwezi mmoja kabla kwa kusafisha, kukarabati au kutengeneza kile unachokihitaji.

VIFAA VINAVYOPASWA KUANDALIWA.
Kabla ya kuanza kufuga nyuki kuna vifaa ambavyo mfugaji wanyukiu anapaswa kuanza kuviandaa mapema kabla ya msimu wa ufugaji wa nyuki kufika.Vifaa hivyo ni kama vifuatavyo:-

UJENZI WA MABANDA YA KUFUGIA NYUKI.
Eneo ambalo kuna wanyama wa aina mbalimbali ambao wanaweza kufanya uharibifu mbalimbali wa mizinga pindi ikiwa na nyuki na kusababisha uharibifu wa mizinga, kuua nyuki au hata mnyama mwenyewe kufa kutokana na kudungwa na nyuki.Hivyo ujenzi wa mabanda ya kufugia nyuki ni vyema ukafanyika.

DHAMIRA YA UJENZI WA MABANDA YA KUFUGIA NYUKI.
Mabanda hayo ya kufugia nyuki yanaweza kuwa ya udongo, tofali au ya miti pekee pande zote, milango pamoja na kuezekwa kwa nyasi.

Kuna sababu mbalimbali ambazo zinasababisha mfugaji nyuki kuweza kujenga mabanda ya kufugia nyuki, miongoni mwa sababu hizo ni:-

1. Kukinga mizinga na jua na mvua.
Hii ni sababu moja wapo ambayo inasababisha mfugaji wa nyuki kuamua kujenga mabanda ya kufugia nyuki, mzinga unapokuwa kwenye kivuli huusaidia mzinga kuweza kudumu kwa kipindi kirefu, pia kivuli husaidia nyuki kufanya kazi zao kwa juhudi.Iwapo mzinga utakuwa upo kwenye jua nyuki hutumia muda mwingi kupunguza joto la ndani ya mzinga badala kutumia muda huo kwa ajili ya kutafuta chakula.

Nyuki wanapoona jua ni kali zaidi na kusababisha joto kali ndani ya mzinga huamua kuhama katika mzinga huo na kwenda kutafuta makazi sehemu nyingine.Hivyo nio vyema mzinga ukakaa kwenye kivuli na sehemu isiyoweza kunyeshewa na mvua.

Pia mvua inaponyeshea mzinga husababisha mbao kuweza kuoza ndani ya muda mfupi, hivyo kwa kujengea banda la kufugia nyuki huweza kuukinga mzinga wako dhidi ya mvua ambayo inasababisha kuozesha mbao za mzinga wako.

2. Kukinga na wanyama waharibifu
Mabanda haya ya kufugia nyuki husaidia sana kwa wanyama waharibifu wa mizinga kushindwa kuifikia mizinga lakini pia husaidia sana kupunguza mashambulizi ya nyuki kwa viumbe wengine.Mizinga huwekwa ndani ya banda na banda kufungwa milango.

3. Ulinzi na ukaguaji
Ujenzi wa mabanda ya kufugia nyuki husaidia sana kuiweka mizinga yako sehemu salama dhidi ya wezi wa mizinga au asali lakini pia husaidia sana wakati wa uangalizi wa mzinga.Mizinga inapokuwa pamoja uangalizi wa mizinga hiyo huwa ni rahisi sana na pia huweza kusaidia kipindi cha uvunaji na uwekaji wa kumbukumbu za kila mara.

Pembeni ya banda hilo sehemu ambazo mizinga inawekwa huwekwa matundu maalumu ya kutoka na kuingia nyuki kwa ajili ya kujitafutia chakula chao.

MIZINGA YA KUFUGIA NYUKI.
Mizinga ya kufugia nyuki inapaswa kuandaliwa mapema kabla ya msimu wa kukamata makundi ya nyuki haujafika.Mizinga inayopaswa kuandaliwa ni kama ifuatayo:-

1. Mzinga wa kibiashara
Huu ni mzinga wa kisasa unaotumika kwa wafugaji wa nyuki hasa wale wanaotaka kuvuna asali kwa wingi kwa ajili ya kuuza.Mzinga huu huweza kuzalisha asali kwa wingi kadri misimu ya uvunaji inavyoongezeka mwaka hadi mwaka.
Mzinga huu una sehemu kuu tatu kama zifuatazo:-

A. Box la kuzalishia watoto wa nyuki
Ni box ambalo kwa kawaida huwa la kwanza kwa upande wa chini.box hili ndilo ambalo huwa na mlandfo wa nyuki kuingia na kutoka pindi wanapokwenda na kutoka kwenye utafutaji wa chakula.Box hili hutumika na malikia wa nyuki kwa kutagia mayai pamoja na kulelea watoto ambao husubiri kuanguliwa na kuwa nyuki kamili.

Pia box hili hutumika kwa ajili ya nyuki kuhifadhia chakula chao kwa ajili ya msimu wa kiangazi, msimu ambao huwa hauna maua yenye chakula cha nyuki cha kutosha,Hivyo mfugaji hapaswi kuvuna asali anayoikuta katika brood box, kwa kuvuna asali unayoikuta katika brood box husababisha kundi lako kuhama kwa kukosa chakula.

Kwa kawaida matumizi ya mzinga huu huanza kuvuna asali baada ya wastani wa misimu miwili mikubwa yaani sawa na miaka miwili.Na mara baada ya kipindi hicho kipita mfugaji huweza kuanza kuvuna kwa vipindi tofauti tofauti vya mwaka na kuendelea.

B. Kitenga malikia
Hiki ni kifaa kama nyavu ambacho huwekwa kati ya brood box na super box, wavu huu huweza kumzuia malikia asiweze kupanda katika super box kwa lengo la kutaga mayai.matundu ya waya huu ni madogo kulingana na umbile la nyuki watenda kazi peke yao.Hivyo malikia na madume ya nyuki hayawezi kupanda kuelekea kwenye super box.

C.  Box la kuhifadhia asali
Hili ni box ambalo huwekwa juu mara tu baada ya queen excluder.Box hili huwa ni maalumu kwa nyuki watenda kazi kuweza kuhifadhi asali yao kwa wingi.Asali inayokuwa katika box hili haiwezi kuchanganyika na watoto wa nyuki wala chavua kutokana na kuwapo kwa queen excluder chini yake.Asali inayotoka katika Box hili huwa nzuri na safi kutokana na kutochanganyika na masega ambayo yalitumika kwa kuangulia watoto wa nyuki.

Uvinaji wa asali katika mzinga huu, mfugaji anapaswa kutoa frame zilizopo katika super box ambazo asali yake tayari imeiva.Mara baada ya kutoa frame hizo mfugaji anapaswa kukamua asali hiyo kwa kutumia mashine ya kisasa iitwayo  Honey Centrifuge Machine.Mashine hii huweza kufyonza asali yote iliyopo katika sega na kubakiza sega likiwa halina asali.

Mara baada ya hapo mfugaji anapaswa kurudisha sega hilo kwenye mzinga likiwa na frame yake ili nyuki aweze kujaza asali tena.Hii inamsaidia sana nyuki kumpunguzia kazi ya kujenga sega jipya la Sali kila baada ya mvuno wa asali na hivyo kuongeza uzalishaji wa asali mara dufu.Tofauti tu ya aina ya mzinga huu ni kwamba huwezi kupata zao la nta.

2. Mzinga wa viunzi
Huu ni mzinga wa teknolojia ya kati kutoka kwenye mizinga ya kienyeji na kuelekea mizinga ya kisasa.Mzinga huu uhifadhi wake wa asali hautofautiani sana na uhifadhi wa asali katika mizinga ya kienyeji, isipokuwa katika mzinga huu masega hupangwa kwa kufuata utaratibu wa viunzi vilivyowekwa.nyuki huweka sega moja katika kila kiunzi kimoja cha mzinga huu.

Mzinga huu pia haujagawanywa kwa kutenganisha sehemu za kuhifadhia asali na sehemu ya malikia kuangulia watoto.Hivyo asali itokayo katika mzinga huu huweza kuchanyanyika na watoto iwapo mfugaji hatakuwa makini katika uvunaji wa asali hiyo.

Uvunaji wa mzinga huu, mfugaji anapaswa kukata sega lote lenye asali pekee na kulihifadhi katika chombo kisafi kwa jili ya kukamua asali hiyo kwa kutumia mashine ya kusasa au kwa kutumia njia za kitamaduni.
Read More

Sunday, 8 January 2017

FAHAMU MIRADI MBALIMBALI UNAYOWEZA KUITUMIA KUTENGENEZA PESA


FURSA 150 ZA MIRADI MBALIMBALI

Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatul, ni matumaini yangu nyote waendelea vyema ndugu msomaji ni jumatatu nyingine tena Alhamdulillah tumepata fursa nyingine ya kuendeleza mapambano
Ifuatayo ni miradi unayoweza itumia kujiongezea kipato

1. Kununua Mashine za kukoroga zege na kukodisha.
2. Kununua Mashine za kukata vyuma na kuzikodisha.
3. Kutengeneza na kuuza tofali
4. Ufundi, Website updating/Database: Katika Halmashauri, Manispaa, Mashule, Wizara, Wilaya na Makampuni mbalimbali.
5.  Kuanzisha kituo cha redio na televisheni
6. Kufunga na kutengeneza vifaa mbalimbali vya electroniki na mawasiliano mfano; compyuta na vifaa vya compyuta na mawasiliano.
7. Kuuza software; mfano Antivirus, Operating Systems, Pastel, Tally, Myob, n.k
8. Kushona na kuuza nguo.
9. Kufungua Duka la kuuza nguo mpya; suit, socks, batiki, nguo za asili, Mashuka, Mashati, Suruali,
10. Ufugaji wa mifugo mbalimbali mfano Kondoo, Mbuzi, Ng’ombe, Kuku, Bata, na wengine.
11. Kufungua stationery, kuuza (supply) vitabu na vifaa mbalimbali ktk mashule na vyuo.
12. Kutoa ushauri mbalimbali wa Kitaalamu.
13. Kuuza viazi, mahindi, mihogo, kutengeneza popcorn na kuziuza.
14. Kusajili namba za simu na kuuza vocha
15. Kuwa na mradi wa Pikipiki zisizotumia mafuta na zinazotumia mafuta
16. Kilimo cha mazao mbalimbali kulingana na hali ya hewa ya sehemu husika.
17. Kuuza Mitumba
18. Kusimamia miradi mbalimbali
19. Kufungua duka la kuuza mitambo mbalimbali
20. Kufungua banda la chakula na chips
21. Kukodisha turubai viti na meza
22. Kufungua Supermarket
23. Kufungua Saluni
24. Kufungua Bucha
25. Video Shooting & Editing.
26. Kufungua Internet cafe
27. Duka la kuuza matunda
28. Kufungua duka la kuuza vifaa vya simu za mkononi na landline.
29. Kufungua duka la vifaa vya ujenzi; cement, vifaa vya umeme, duka la mabati
30. Kutengeneza michoro mbalimbali ya majumba na miradi ya ICT
31. Kuchapa vitabu, bronchures, n.k
32. Kuanzisha kampuni ya ujenzi (Building contractor)
33. Kuuza Vifaa vya umeme wa nishati ya jua (solar) ,battery, inverter na vifaa vingine vya solar n.k
34. Kuuza maji kwa jumla na rejaleja.
35. Kutengeneza na kuuza Unga wa lishe bora.
36. Kukodisha Music
37. Kuanzisha Mradi wa Taxi
38. Kuanzisha mradi wa Daladala
39. Kuuza vifaa vya Kompyuta, laptops, converters, HDDs, Monitors, Softwares, CD Copiers na vifaa vingine.
40. Kununua magenerator na kukodisha
41. Kufungua kampuni ya kutoa huduma za simu
42. Kufungua kampuni ya kutoa huduma za internet (ISP)
43. Kuuza mabati na vigae
44. Kujenga apartments
45. Kufungua Kisima cha mafuta ya taa au mafuta ya aina zote
46. Kufungua Duka la samaki
47. Kufungua Duka la nafaka
48. Kufungua Shule za Awali, Shule za Msingi, Sekondari na Vyuo.
49. Kujenga hostel
50. Kuuza vocha na ving’amuzi vya DStv, Zuku, Startimes, Easy TV, TNG, Digitech, Continental.
51. Kujenga mtambo wa kuzalisha umeme na kuuza katika viwanda na wananchi.
52. Ufundi simu
53. Kufungua Hospitali, Zahanati.
54. Maabara ya Macho, Meno
55. Kuchimba/Kuuza Madini
56. Kufungua ofisi ya kutoa huduma ya simu na fax
57. Kuuza miti na mbao
58. Kufungua Grocery, bar
59. Kufungua studio ya kupiga na kusafisha picha
60. Kucharge simu/battery
61. Duka la TV na vifaa vingine
62. Kuanzisha biashara ya kuuza vyakula katika sherehe na tamasha mbalimbali (catering).
63. Banda la kupigisha simu
64. Kuuza na kushona Uniform za shule
65. Kuanzisha duka la kuuza vitu kwa jumla.
66. Kufungua gereji za kutengeneza bajaji, pikipiki na magari
67. Kuuza vyuma, pembejeo, rake, jembe
68. Kuuza fanicha
69. Kufungua sehemu ya kuziba pancha za matairi
ya magari na mitambo.
70. Kujenga nyumba za kulala wageni (hotel)
71. Kuagiza na kuuza vifaa vya aluminium.
72. Kuuza vioo
73. Kushona na kukodisha nguo za harusi
74. Kufungua yard kwa ajili ya kuosha magari
75. Kuuza mashine za kuchomelea (welding machine).
76. Kuuza vifaa vya kuvaa Site (boots, helmets etc)
77. Kununua mabasi kwa ajili ya kusafirisha wanafunzi
78. Kufungua studio ya kutengeneza vipindi vya redio na televisheni
79. Kuanzisha ofisi ya michezo ya televisheni (TV Games)
80. Kufungua benki
81. Kuwa na malori ya kubeba kokoto na mchanga
82. Kuuza vifaa mfano TV, CCTV Camera, n.k
83. Kuwa dalali wa vitu mbalimbali
84. Kuanzisha mradi wa kukodisha fork lift na winchi (crane)
85. Kuanzisha kiwanda cha kutengeneza viatu.
86. Kuanzisha viwanda mbalimbali
87. Duka la vifaa vya simu na gadgets mbalimbali zinazoendana na mawasiliano ya Vodacom, TTCL, AIRTEL, TIGO, ZANTEL, n.k.
88. Kujenga Ukumbi wa kukodisha kwa sherehe, mikutano mbalimbali
89. Kununua matrekta, mitambo ya ujenzi wa barabara na kukodisha
90. Kutengeneza antenna na kuuza
91. Kufungua mradi wa Machine za kusafisha, kutoboa na kuchana mbao
92. Kufungua mradi wa kuuza vifaa vya Umeme wa kutumia upepo
93. Biashara ya kuagiza magari
94. Kufanya biashara za Jukebox
95. Kukodisha matenki ya maji
96. Kufungua duka la kuuza Asali
97. Kutengeneza Mikokoteni/ matoroli na kuikodisha
98. Kufungua Duka la vinyago, batiki
99. Kuanzisha huduma ya AIRTEL MONEY, MPESA, TIGOPESA, EZY PESA
100. Kuanzisha sehemu ya kufanyia mazoezi (Gym).
101. Kununua na kuuza vifaa vya kupima ardhi.
102. Kufungua duka la kuuza dawa (pharmacy).
103. Kufungua Kampuni ya Ulinzi
104. Kufungua kampuni ya "Clearing and fowarding"
105. Kuchezesha vikaragosi
106. Kuuza spea za bajaji, magari na pikipiki
107. Kuuza baiskeli
108. Kuuza magodoro
109. Kuuza vyombo mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya nyumbani mfano bakuli, sahani, vikombe, vijiko,
110. Kuuza marumaru (limestones)
111. Kuuza kokoto
112. Kuuza mchanga
113. Kufundisha Tuisheni
114. Biashara za bima
115. Kampuni ya kusafirisha abiria kwa njia ya anga (ndege)
116. Biashara za kitalii
117. Biashara za meli na maboti.
118. Kampuni ya kuchimba visima
119. Kufungua ofisi ya wakili/mawakili wa kujitegemea
120. Kuuza mkaa
121. Kutengeneza mashine za kutengeneza tofali
122. Kampuni ya kupima ardhi
123. Kampuni ya magazeti
124. Kuchapa (printing) magazeti
125. Kuuza magazeti
126. Kuchimba mafuta
127. Kiwanda cha kutengeneza mabati
128. Kiwanda cha kutengeneza fanicha
129. Kiwanda cha kutengeneza matairi
130. Kutengeneza vitanda vya chuma
131. Kununua nyumba katika Maghorofa (Apartments) na kuzikodisha.
132. Kukodisha makapeti
133. Kupamba maharusi na kumbi za harusi/sherehe.
134. Mashine ya kusaga na kukoboa nafaka.
135. Kazi ya ususi na kusafisha kucha.
136. Kuuza Gypsum
137. Malori ya kubeba mafuta na Mizigo
138. Duka la kuuza mboga za majani
139. Duka la kuuza maua.
140. Kampuni ya kuzoa takataka
141. Kampuni ya kuuza magari
142. Kuuza viwanja
143. Uvuvi
144. Kutengeneza na kuuza nguzo za kujengea fensi
145. Uchoraji wa mabango.
146. Duka la kuuza silaha
147. Ukumbi wa kuonesha mpira
148. Biashara ya mlm (network marketing)
149. Yadi kwa ajili ya kupaki magari
150. Mradi wa trekta za kukodisha kwa ajili ya kilimo
Read More