Monday, 3 October 2016

JIFUNZE KUVUMILIA ILI UPATE KUNG'ARA


JIFUNZE KUVUMILIA YOTE ILI UNG’ARE

Alhamdulillah ni siku nyingine tena na ninaimani sote tumeamka salama tumshukuru Allah Kwa zawadi hii ya uzima,awali ya yote napenda kukuuliza hivi  Umewahi kujiuliza kwanini unaogopa sana kufanya kitu ulichopanga kukifanya kwa muda mrefu sasa ingawa unajua kabisa ni jambo jema kufanya na iwapo ukilifanya maisha yako yatavuka hatua nyingine muhimu na kuwa bora zaidi. Kila mara unapotaka kuanza kulifanya unajikuta unajiambia ni bora usubiri maana ukianza kulifanya hilo kwa muda huo lazima utashindwa. Matokeo yake ni kila siku umekuwa mtu wa kusitisha kufanya au unaanza unaishia katikati. Wakati mwingine umeanza kujilaumu na kujiona ni mtu ambaye huwezi kufanikiwa tena juu ya hilo.
Majibu ya sababu za hali hii yako mengi ila leo naomba nizungumze nawewe juu ya sababu moja inayochangia unashindwa kusogea mbele. Sababu hiyo ni kuwa uwezo wako wa kuvumilia mateso ya kukipata hicho kitu bado uko chini. Saikolojia ya mwanadamu inaweka wazi kuwa katika chochote unachotaka kukifanya sehemu ya ubongo wako inayohusika na matendo yasiyo ya hiari (unconscious mind) hupima kiwango cha mateso utakayo yapata kwa kufanya au kutokufanya hilo unalotaka kulifanya ikilinganisha na furaha utakayopata kwa kufanya au kutokufanya jambo hilo. Pale ambapo mateso yanapoonekana kuwa ni mengi kuliko furaha utakayopata unajikuta tayari umeamua kuahirisha kufanya ulichotaka kufanya pengine bila hata wewe mwenyewe kujiuliza.
Lakini pia saikolojia inaendelea kusema kuwa sehemu hii ya ubongo mara zote hutumia uzoefu wa taarifa za nyuma ulizowahi kuzipata ili kuchukua maamuzi wakati wa kupima kiwango cha furaha na mateso juu uamuzi unaouchukua. Hili linatupa nafasi ya kutambua kuwa kila mara tunapoanguka kuwa si kweli kuwa hatuna nguvu za kuendelea mbele na kufanya vizuri Zaidi bali ni kuwa hatuko tayari kuvumilia mateso tunayoyaona mbele tukilinganisha na furaha ya kuacha kufanya hilo.
Kitu kibaya ni kuwa maamuzi haya hufanyika bila ya sisi wenyewe kuhusishwa na baadae hupokea matokeo, lakini nafasi tuliyonayo ni kuuongeza uzoefu wetu juu ya uvumilivu wa mateso tunapoamua kufanya jambo ukilinganisha na furaha ya kitambo pale tutakapoamua kutokufanya. Ni lazima kama watu tuliodhamilia kushinda kuhakikisha nguvu yetu ya kuamini juu ya uvumilivu wa mateso ni kubwa kuliko upendo wa furaha ya kitambo, kila siku hakikisha unapata hamasa ya kukufanya kunasogea mbele mateso na kuvuka.
Mwandishi maarufu wa kimarekani Zig Ziglar aliwahi kusema “People often tell me that motivation doesn’t last. And I tell them that bathing doesn’t either. That’s why I recommend daily.” yaani “watu huniambia uhamasishaji hauishi, nami huwaambia ndivyo ilivyo kuoga pia. Hiyo ndio sababu ninasitiza iwe kila siku.” Alijua kama ulivyo mwili unawili na kupendeza huhitaji kusafishwa na maji safi kila siku ndivyo  ilivyo pia nia (mind) ya mwanadamu inahitaji kulishwa mema kila siku ili iamue mema. Kuanzia leo jifunze kuushibisha ubongo wako maneno ya kutia moyo na kuamini ushindi unawezekana ili ushinde. Ukuze uwezo wako wa kuvumilia mateso utatoka ulipokwama.
Wewe ni mshindi,mwamshe shujaa ndani yako.

NAOMBA UTEMBELEE BLOG YANGU HII naythambis.blogspot.com UPATE KUJIFUNZA MAMBO MBALIMBALI PIA KWA USHAURI NAOMBA UNIANDIKIE UJUMBE KUPITIA +255689538628/nsalum998@gmail.com
#POSITIVETHOUGHT
#STRUGGLESREAL
#DREAMBIG
Read More

KISICHOKUUA HUKUPA NGUVU, USIKATE TAMAA!

CHANGAMOTO ZAKO ZA KIMAISHA SIYO MWISHO WA MAISHA YAKO

Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatul mpendwa msomaji wa blog hii, ni matumaini yangu upo vizuri SHUKRANI KWA ALLAH KWA KUTUPA UZIMA,baada ya kimya nimerudi tena naomba tuendelee kujifunza

Asilimia kubwa ya watu hupenda kukata tamaa na maisha Baada ya kukutana na changamoto mbalimbali za kimaisha hali ambayo inawapelekea kuishi maisha ya kinyonge na wakati mwingine kuishia kufanya maamuzi ambayo yanaweza kuwasababishia madhara ya kudumu katika maisha yako

Kwanini tunakumbana na changamoto nyingi za kimaisha...?
Kuna sababu nyingi sana ambazo zinatusababisha tukumbane na changamoto nyingi za kimaisha katika maisha yetu ya kila siku na miongoni mwa sababu hizo ni kama zifuatazo

1. Mgawanyiko katika familia
Matatizo mengi katika familia zetu za kiafrika yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na familia zetu ambapo ni jambo la kawaida kukuta ndugu wakibaguana,  wakidhalilishana, wakichukiana,  wakisemana vibaya na kufanyiana vitendo ambavyo havitakiwi kufanyiana

Imekuwa ni jambo la kawaida kwa mwanafamilia mwenye uwezo wa kumsaidia mwanafamilia mwingine kushindwa kumsaidia mwanafamilia huyo kwa makusudi pamoja na kuwashawishi watu wengine wasimsaidie huyo mwanafamilia kwa kuwaaminisha kuwa kumsaidia huyo mtu ni kupoteza mda wao pamoja na pesa zao
Hali ya kushindwa kusaidiana kwa wanafamilia inachangia kwa kiasi kikubwa baadhi ya watu kutafuta namna nyingine ya kufanikisha malengo yao bila ya kutegemea msaada wa aina yoyote kutoka katika familia hali ambayo inawafanya waishie kujitenga na familia zao

Madhara ya Mgawanyiko katika familia yanaweza yakachangia kwa kiasi kikubwa matabaka katika familia pamoja na kuondoa hali ya kusaidiana na kushirikiana katika shida na raha hali ambayo itaondoa upendo katika familia

2. Ubinafsi
Kuna baadhi ya watu ambao wanapenda waonekane bora kushinda wenzao pamoja na kutengeneza mazingira ya kuogopewa na wenzao pamoja na kutokukosolewa au kushauriwa katika jambo lolote katika maisha yao jambo ambalo linapelekea kwa kiasi kikubwa kugombana na yoyote ambaye atajaribu kumkosoa kwa namna yoyote au kumshauri jambo lolote

Mara nyingi watu wabinafsi wapo teyari kufanya lolote kwa ajili ya kulinda nafasi zao katika jamii pamoja na vyeo vyao au kumtumia mtu yoyote kwa ajili ya kufanikisha malengo yao bila ya kujali athari ambazo atazipata mtu ambaye watamtumia kufanikisha mipango yao

Mtu mbinafsi yupo teyari kukusababishia matatizo kwa ajili ya Manufaa yake wakati wowote pale anapopata Fursa ya kufanya hivyo bila ya kujali madhara yoyote utakayoyapata

3. Tamaa
Wakati mwingine tamaa ya kupenda vitu vizuri pamoja na mafanikio ya Haraka bila kujali njia unazozitumia katika kupata hivyo vitu vizuri na hayo mafanikio ya Haraka inaweza ikakufanya ujikute katika matatizo mbalimbali na kupelekea kuishia katika Mikono ya sheria au kupitia katika mateso, udhalilishwaji na Kutumika na watu wachache katika Manufaa yao

Ni vizuri kujaribu kuzishinda baadhi ya tamaa na kujaribu kupanga mikakati pamoja na mipango ya kimaisha ambayo itakufanya uishi kwa Amani bila ya hofu ya kuishia katika Mikono ya kisheria au Kutumika katika kwa ajili ya Manufaa ya watu wachache huku wewe ukiangamia

4. Kutokujiamini
Haijalishi una mipango mizuri kiasi gani, mbinu nzuri kiasi gani au kipaji kiasi gani.. kama ukishindwa kujiamini basi mipango yako, kipaji chako na mbinu zako hazitaweza kukusaidia katika maisha, ikumbukwe kwamba kujiamini pamoja na uelewa sahihi wa jambo unalotamani kulifanikisha ni silaha muhimu inayohitajika katika kufanikisha jambo lolote katika maisha.

Kutokujiamini kunaweza kukusababishia matatizo mbalimbali kama vile Kutumika na baadhi ya watu kwa Manufaa yao, kudhulumiwa, kuchezewa pamoja na kufanyiwa vitu mbalimbali visivyostahili na baadhi ya watu unaowategemea wakusaidie kwasababu wanaamini kuwa uwezi kufanikisha lolote bila ya wao

Ni muhimu Kuanza kujiamini katika mambo unayotamani kuyafanikisha pamoja na kujitahidi kujifunza mambo mbalimbali yatayokusaidia kuwa na uelewa wa kutosha kuhusiana na mambo unayotamani kuyafanikisha.

5. Kutomshirikisha Mungu katika Mipango yako
Watu wengi ambao hawakati tamaa katika maisha wanatabia ya kumshirikisha Mwenyezi Mungu katika mipango yao ya kimaisha ambapo inapotokea wanakwama katika mipango yao uamini kuwa muda wao wa kufanikisha mipango yao haujafika na ukifika ni lazima wafanikiwe kwa kiasi kikubwa ambapo kutofanikiwa kwao katika jambo flani ndio Fursa yao ya kujifunza wapi walipokosea pamoja kutambua mapungufu yao kwa ajili kufanya vizuri watakapojaribu kwa mara nyingine

Unaposhindwa kumshirikisha Mwenyezi Mungu katika mipango yako unaweza kuishia kuwalaumu watu pamoja na kugombana na watu mbalimbali unaoamini kuwa wanakuhujumu kwa namna moja au nyingine bila ya kutafuta suluhisho bora la jinsi ya kufanikisha malengo yako.

6. Uoga
Uoga ni tatizo ambalo linawasababishia matatizo makubwa watoto wadogo, vijana, watu wazima, wazazi, wafanyakazi mbalimbali pamoja na watu mbalimbali waliojiajiri, wakati mwingine madhara ya uoga yanaweza yakawasababishia matatizo mbalimbali hata watu wasio na hatia

Mfano mdogo ni pale mtu anapojichanganya kwasababu ya hofu na kutoa ushahidi au maelezo yanayopishana mahakamani na kuvuruga ushahidi mzima na kumyima mtu mwingine haki yake ambayo ilikuwa ikitegemea ushahidi wake, hali hii pia inajitokeza kwa watoto ambao ufanyiwa vitendo vya kidhalilishaji na ndugu zao hususani wajomba zao na kuogopa kuwasemea kwa Wazazi wao kutokana na uoga wao

Uoga una madhara moja kwa moja kwa anayeogopa ambapo anaweza kupata madhara makubwa kwa kushindwa kuwa muwazi katika matatizo yake aliyonayo, mfano mtu anapoogopa kuwa wazi kuhusu ugonjwa alionao anaweza akijikuta akipata madhara makubwa badae au kushindwa kutibika kirahisi pale ugonjwa wake unapofikia katika hatua kubwa ambapo awali angeweza kutibika kama angekuwa muwazi katika hatua za awali

Kwa upande mwingine madhara ya uoga yanaweza kuwagusa hata watu wengine wasiokuwa na hatia kwa mfano pale mtu anapoamua kumuhujumu mwenzake ili yeye aendelee kuwa katika nafasi nzuri ya kufanikisha jambo flani au kumuharibia mtu mipango yake kwa makusudi kwa kuogopa kuwa huyo mtu anaweza kufanikiwa na wakati mwingine uoga uweza kuwasababishia watu msongo wa mawazo katika maisha yao kwa vitu ambavyo vinaweza kuepukika.

Tatizo la uoga kwa kiasi kikubwa linaweza kutatuliwa kwa kujiamini, kutafuta taarifa sahihi katika jambo unalotamani kulifanikisha pamoja na kujitahidi kuwa karibu na watu watakaokusaidia kukujengea hali ya kujiamini

7. Uongo
Hakuna kitu ambacho kinaweza kuwagombanisha watu kwa urahisi pamoja na kuondoa hali ya kuaminiana kama Uongo, Ikumbukwe kuwa mara nyingi vitu vya Uongo uwa vinasambaa kwa kasi Sana kuliko mambo ya kweli na wakati mwingine kuaminika kirahisi kuliko mambo ya kweli

Mara nyingi unaposingiziwa mambo ya Uongo, unaweza usiaminike kwa kipindi flani katika maisha yako kwa sababu ya kuaminika kuwa ni kweli umefanya jambo uliosingiziwa wakati siyo kweli
Haijalishi utasingiziwa mambo mangapi katika maisha,  elewa kwamba ipo siku ukweli utabainika na wewe utasafishwa dhidi ya Uongo wote ulioenezwa juu yako

8. Mazingira tunayoishi
Wakati mwingine mazingira tunayoishi yanaweza kutengeneza changamoto katika kufanikisha ndoto zetu kutokana na Kukosekana kwa mazingira rafiki ambayo yangeweza kutuunganisha na wadau mbalimbali ambao wangetusaidia katika kuendeleza vipaji vyetu pamoja na kutusaidia kutimiza ndoto zetu

Unapokuwa katika mazingira ya aina hii unatakiwa usikate tamaa zaidi ya kutumia njia mbadala za kuwafikia wadau unaoamini kuwa wanaweza kuwa msaada kwako katika kutimiza malengo yako, baadhi ya njia hizo ni kama mitandao ya kijamii, simu, barua pepe pamoja na kuhudhuria semina na makongamano mbalimbali yatakayokuweka karibu au kukuunganisha na hao wadau

9. Aina ya Marafiki au watu unaoshirikiana nao
Karibia kila mtu amekuwa na vigezo vyake katika kutafuta mchumba au Mume/Mke kabla ya kuamua kuwa mchumba wa mtu flani au mke/Mume wa mtu flani lakini kwa kiasi kikubwa wengi wetu tumekuwa hatuna vigezo linapokuja suala la kuchagua rafiki wakati mda mwingine tumekuwa tukiwaamini marafiki zetu kwa kuwaeleza mambo yetu mbalimbali ambayo hatuwezi kuthubutu kuwaambia wachumba zetu au Mke/Mume

Ikitokea ukawa na marafiki wasio waaminifu au kushirikiana na watu ambao siyo waaminifu basi kuna uwezekano wa asilimia kubwa maisha yako yakakubwa na changamoto mbalimbali zitokanazo na usaliti kutoka kwa marafiki zako au watu utakaoshirikiana nao

Ni vizuri kuwa na tabia ya kujiridhisha kwanza katika mambo mbalimbali kabla ya kuamua kumshirikisha mtu katika mipango yako mbalimbali

10. Kushindwa kuaminiana
Unaposhindwa kuaminika katika mambo unayotaka kuyafanya unakuwa katika changamoto kubwa ya kutafuta njia nyingine mbadala ya kuhakikisha kuwa unatimuza ndoto zako, hali uwa inawakatisha sana tamaa baadhi ya watu kuendelea na mipango yao

Tatizo la kushindwa kuaminiana mara nyingi linaanzia katika familia ambapo baadhi ya wanafamilia upenda kuwachagulia wanafamilia wenzao vitu vya kusomea na aina ya kazi wanazozitaka wao hali ambayo uleta changamoto pale anayechaguliwa kazi na masomo na wanafamilia wenzake anapokuwa na mawazo tofauti

11. Ushirikina
Mara nyingi unapokosa hofu ya Mungu ni rahisi kukata tamaa katika maisha yako pamoja na kuingia katika imani za kishirikina kwa kuamini kuwa unaweza kufanikisha ndoto zake kupitia msaada wa nguvu za giza
Unapoanza kutumia nguvu za giza ni rahisi kuwadhulu wengine kwa kutumia nguvu za giza pamoja na kuwasababishia matatizo mbalimbali kulingana na masharti utakayopewa

Ni vizuri kujiamini pamoja na kumuamini Mungu ili uweze kufurahia mafanikio yasiyokuwa na masharti yoyote wala kuwasababishia matatizo mengine

Imeandikwa na NAYTHAM S MASOUD
06895386286/nsalum998.gmail.com
TAFADHALI SHARE NA RAFIKI ZAKO WAPATE KUJIFUZA
Read More

Saturday, 1 October 2016

JE, WEWE NI MJASIRIAMALI?? JENGA MSINGI IMARA WA BIASHARA YAKO!!


Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatul, natumai mnaendelea vizuri leo napenda kukufunza namna ya kujenga msingi imara wa biashara yako, inawezekana una biashara yako Lakini inaonekana kufa au unataka kuanzisha biashara unahofia kupata hasara basi tambua bado hujafanikiwa kujenga msingi wa biashara yako
~rafiki tambua kuwa ni muhimu kujenga msingi imara wa biashara kama ilivyo muhimu kujenga msingi imara wa nyumba, rafiki ni muhimu kujenga msingi imara wa biashara lasvyo biashara yako inaweza kufa na ukapata hasara
~na katika kila msingi utakaouweka basi tambua Kuna sehem mbalimbali ambazo unatakiwa uhakikishe zipo imara haswa ili biashara yako iweze kukua vizuri kwasababu inaweza kuwa mtaji umekopa hivyo yakupasa kupangilia vizuri ili uweze kurudisha mkopo na kukuza biashara yako unapaswa uwe na msingi imara wa matumizi na kusave, pia ni lazima ujue kuwa biashara unayotaka kuanzisha au unayofanya na ujue wateja wako wanapatikana wapi na lazima uhakikishe kila senti tano inayotoka inaenda wapi na unaifanyia nini pia hakikisha unatunza kumbukumbu vizuri kwa kuwa lengo la kuanzisha biashara ni kuwa kiongozi wa biashara yako hivyo ni lazima ujenge msingi mzuri wa kutoa huduma bora kwa wateja wako na uhakikishe kila mmoja anaridhika na huduma yako na ukiona huwaridhishi fanya kila linalowezekana ili waridhike na kufurahia biashara yako
RAFIKI HAKIKISHA UNAJENGA MSINGI IMARA WA BIASHARA YAKO ILI IWEZE KUDUMU
WASILIANA NAMI 0689538628 KWA USHAURI NA MAWAZO JUU YA BIASHARA
Read More