JIFUNZE KUVUMILIA YOTE ILI UNG’ARE
Alhamdulillah ni siku nyingine tena na ninaimani sote tumeamka salama
tumshukuru Allah Kwa zawadi hii ya uzima,awali ya yote napenda kukuuliza
hivi Umewahi kujiuliza kwanini unaogopa sana kufanya kitu ulichopanga
kukifanya kwa muda mrefu sasa ingawa unajua kabisa ni jambo jema kufanya
na iwapo ukilifanya maisha yako yatavuka hatua nyingine muhimu na kuwa
bora zaidi. Kila mara unapotaka kuanza kulifanya unajikuta unajiambia ni
bora usubiri maana ukianza kulifanya hilo kwa muda huo lazima
utashindwa. Matokeo yake ni kila siku umekuwa mtu wa kusitisha kufanya
au unaanza unaishia katikati. Wakati mwingine umeanza kujilaumu na
kujiona ni mtu ambaye huwezi kufanikiwa tena juu ya hilo.
Majibu ya sababu za hali hii yako mengi ila leo naomba nizungumze nawewe
juu ya sababu moja inayochangia unashindwa kusogea mbele. Sababu hiyo
ni kuwa uwezo wako wa kuvumilia mateso ya kukipata hicho kitu bado uko
chini. Saikolojia ya mwanadamu inaweka wazi kuwa katika chochote
unachotaka kukifanya sehemu ya ubongo wako inayohusika na matendo yasiyo
ya hiari (unconscious mind) hupima kiwango cha mateso utakayo yapata
kwa kufanya au kutokufanya hilo unalotaka kulifanya ikilinganisha na
furaha utakayopata kwa kufanya au kutokufanya jambo hilo. Pale ambapo
mateso yanapoonekana kuwa ni mengi kuliko furaha utakayopata unajikuta
tayari umeamua kuahirisha kufanya ulichotaka kufanya pengine bila hata
wewe mwenyewe kujiuliza.
Lakini pia saikolojia inaendelea kusema kuwa sehemu hii ya ubongo mara
zote hutumia uzoefu wa taarifa za nyuma ulizowahi kuzipata ili kuchukua
maamuzi wakati wa kupima kiwango cha furaha na mateso juu uamuzi
unaouchukua. Hili linatupa nafasi ya kutambua kuwa kila mara
tunapoanguka kuwa si kweli kuwa hatuna nguvu za kuendelea mbele na
kufanya vizuri Zaidi bali ni kuwa hatuko tayari kuvumilia mateso
tunayoyaona mbele tukilinganisha na furaha ya kuacha kufanya hilo.
Kitu kibaya ni kuwa maamuzi haya hufanyika bila ya sisi wenyewe
kuhusishwa na baadae hupokea matokeo, lakini nafasi tuliyonayo ni
kuuongeza uzoefu wetu juu ya uvumilivu wa mateso tunapoamua kufanya
jambo ukilinganisha na furaha ya kitambo pale tutakapoamua kutokufanya.
Ni lazima kama watu tuliodhamilia kushinda kuhakikisha nguvu yetu ya
kuamini juu ya uvumilivu wa mateso ni kubwa kuliko upendo wa furaha ya
kitambo, kila siku hakikisha unapata hamasa ya kukufanya kunasogea mbele
mateso na kuvuka.
Mwandishi maarufu wa kimarekani Zig Ziglar aliwahi kusema “People often
tell me that motivation doesn’t last. And I tell them that bathing
doesn’t either. That’s why I recommend daily.” yaani “watu huniambia
uhamasishaji hauishi, nami huwaambia ndivyo ilivyo kuoga pia. Hiyo ndio
sababu ninasitiza iwe kila siku.” Alijua kama ulivyo mwili unawili na
kupendeza huhitaji kusafishwa na maji safi kila siku ndivyo ilivyo pia
nia (mind) ya mwanadamu inahitaji kulishwa mema kila siku ili iamue
mema. Kuanzia leo jifunze kuushibisha ubongo wako maneno ya kutia moyo
na kuamini ushindi unawezekana ili ushinde. Ukuze uwezo wako wa
kuvumilia mateso utatoka ulipokwama.
Wewe ni mshindi,mwamshe shujaa ndani yako.
NAOMBA UTEMBELEE BLOG YANGU HII naythambis.blogspot.com UPATE KUJIFUNZA
MAMBO MBALIMBALI PIA KWA USHAURI NAOMBA UNIANDIKIE UJUMBE KUPITIA
+255689538628/nsalum998@gmail.com
#POSITIVETHOUGHT
#STRUGGLESREAL
#DREAMBIG